KESI ya kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na kauli yake ya kuruhusu wanaokaidi maagizo ya Dola wapigwe, itatajwa Septemba 16 mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo ilifunguliwa Agosti mosi mwaka huu na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), dhidi ya Waziri Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wakipinga kauli hiyo
↧