MIHADHARA ya dini iliyokuwa imepigwa marufuku na Serikali imeruhusiwa
kuendelea kwa masharti ya kutojihusisha na mahubiri yanayolenga
kupandikiza chuki miongoni mwa Wakristo na Waislamu. Serikali pia
imewataka viongozi wote wa dini kuwakataa na kuwapiga marufuku watu
wanaojiingiza katika nyumba za ibada huku wakiwa na malengo ya siasa.
Akizungumza katika kongamano la Umoja wa Wahadhiri
↧