Aliyekuwa rais wa marekani Bill Clinton amempongeza
rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mafanikio ya nchi yake licha ya madai kwamba amekuwa akiunga mkono
makundi ya waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo
yanakiuka haki za kibinadamu.
Bwana Clinton amesema katika mahojiano na BBC kwamba madai hayo ambayo Rwanda inayakataa hayajathibitishwa mahakamani.
↧