Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limelaani vikali
tukio la polisi kumjeruhi Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu,
Sheikh Issa Ponda na limetaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza tukio
hilo huku likimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile kujiuzulu.
Ponda amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili
(Moi), akitibiwa majeraha yanayoaminika kuwa ya risasi
↧