Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga
simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia
uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa
sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu
mbovu na madhara yake katika mawasiliano
↧