Mzozo wa wapenzi wawili usiku, umesababisha mmoja wa kike kupiga mayowe
ya kumuita mwenzake mwizi, akavamiwa na watu waliompiga na kumchoma moto
hadi kufa.
Kisa hicho kimetokea mkazi wa Magazini mjini Mpanda mkoani Katavi,
Florence Mabuga (29), ambaye baada ya kuvamiwa na watu akidhaniwa mwizi,
alipigwa na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto mbele ya nyumba yake.
↧