SERIKALI katika mkoa wa Kusini Unguja, imemtimua kazi Sheha wa Kitumba,
Mtwana Kificho, ambaye wiki iliyopita nyumbani kwake alikutwa na majani
makavu yanayosadikiwa kuwa bangi baada ya polisi kufanya ukaguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dk
Idrissa Muslim Hijja, jana aliwateuwa masheha wawili na kuwaapisha
kuongoza shehia hizo, pamoja na sheha mpya wa Kitumba, Makame Chum.
↧