Mauaji, mashambulizi ya kudhuru mwili na uporaji vimeendelea
kuchafua taswira ya Tanzania baada ya juzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao
hawajafahamika, raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali na
mfanyabiashara kuporwa zaidi ya Sh40 milioni.
Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda Hospitali ya
Aga Khan kuwajulia hali raia hao
↧