Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe kwa wale wanaoitishia
Tanzania. Amewaambia wakithubutu watakiona cha mtemakuni kama ilivyokuwa
kwa Idd Amin wa Uganda.
Alisema mamlaka za ulinzi na usalama zilimdhibiti
Amin alipofanya uvamizi katika ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba
hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingine yeyote atakayechezea
usalama wa nchi.
↧