Mahakama ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imewahukumu raia watatu kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenda jela miaka 15 au kulipa faini ya Sh milioni tatu kwa wote baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na gunia mbili za bangi kavu yenye uzito wa kilo 50.
Washtakiwa hao Kasangu Paul (40), Mkambala Mwabu (39) na Kiwele Msaka (32) wote kutoka katika Mji wa Moba nchini DRC
↧