Polisi aliyejiua kwa kujipiga risasi mdomoni, Aloyce Mafuru
(24), amezikwa katika makaburi ya Mugumu, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa
Mara bila huduma za kidini na kijeshi.
Askari huyo aliyekuwa dereva wa Kamanda wa Polisi
Wilaya ya Manyoni, Alute Makita alijiua Februari 2 nyumbani kwake na
kuacha ujumbe kuwa polisi wasiangike kufanya uchunguzi kwani huo ni
uamuzi wake binafsi.
↧