SERIKALI imesisitiza agizo lake la kusitisha ujenzi wa ofisi za wizara na taasisi zake katika jiji la Dar es Salaam badala yake uelekezwe mjini Dodoma, ikiwa ni hatua ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma.
Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chilonwa, Ezekiah Chibulunje (CCM)
↧