FEDHA zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kiuchumi maarufu kama mabilioni ya Kikwete, imeelezwa sehemu hazikutumika huku nyingine zilizokopwa hadi sasa hazijarejeshwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza alitoa taarifa hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Salumu Msabaha (Chadema).
↧