Askari wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na majambazi, waliovamia kituo hicho na kuiba silaha baada ya kufanikisha mauaji.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi liko katika msako mkali, huku Mkuu wa jeshi hilo, IGP, Ernest Mangu akitangaza donge nono la Sh milioni 20 kwa watakaofanikisha kukamatwa
↧