MAJAMBAZI watano wakiwa na silaha za moto na mapanga wamevamia duka la fedha la Mji mdogo wa Sirari na kupora Sh milioni 45 za Kitanzania na fedha za Kenya elfu 50.
Katika hekaheka hizo majambazi hao wamejeruhi watu wawili akiwemo mwalimu wa shule ya msingi Sirari anayeitwa Mataigwa Muhono (30) aliyepigwa risasi mguuni na mdogo wa mwenye duka ambaye alikuwa akitoa huduma Mara Masabi (23)
↧