Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Maputo, mji mkuu wa Mozambique, usiku
wa Jumatano, Januari 14, 2015, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais
mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi.
Sherehe zinafanyika Independence Square, mjini Maputo leo, Alhamisi,
Januari 15, 2015. Mheshimiwa Nyusi anakuwa Rais wa nne wa Mozambique
tokea uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975.
↧