Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account, kuna mtu au
kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya
mtandao wa Twitter kwa jina la Edward Ngoyai Lowassa, @edwardlowasa.
Kwa
kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa
kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea
bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Mhe. Lowassa.
↧