Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya
usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki
dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa,
ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki
dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.
↧