Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche (22), aliushangaza umma uliohudhuria maafali ya 44 ya chuo hicho baada ya kutangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science).
Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango
↧