Makatibu wakuu wa CCM, Abulrahman Kinana na Dk Willibrod Slaa wa
Chadema kesho watashiriki katika mjadala wa rais wa Tanzania
anayetakiwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mjadala
huo utakaofanyika Dar es Salaam, umeandaliwa na Asasi ya Twaweza ikiwa
ni sehemu ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa maoni ya wananchi juu ya
mwelekeo wa rais wanayemtaka kupitia uchaguzi wa mwaka 2015.
↧