HALI ya Rais Jakaya Kikwete ambaye mwishoni mwa wiki alifanyiwa operesheni ya tezi dume, inaendelea kuimarika na ameanza kufanya mazoezi ya kutembea.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya kufanyiwa operesheni ya tezi dume kwenye Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani.
↧