SERIKALI imesema itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria na za kinidhamu madaktari wote watakaogundulika kujihusisha na utoaji wa mimba kinyume na utaratibu.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Dimani, Abdallah Sharia Ameir (CCM) kwa niaba ya
↧