TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeanza uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa Sh bilioni 40, uliotajwa kufanyika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk Edward Hoseah alisema jijini Mwanza jana kuwa tayari timu ya wachunguzi 148 wameshawasili jijini kuanza uchunguzi huo ambao umekwishaanza, ingawa hakuweka bayana timu hiyo itakamilisha lini
↧