MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru wafanyabiashara watatu, wakiwemo mume na mke, waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 13 na miezi sita jela kwa sababu ya wizi wa Sh bilioni 1.1 katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Walioachiwa huru ni mume Manase Makale na mkewe Edda Makale, na mfanyabiashara mwingine Bahati Mahenge.
↧