MKOA wa Kilimanjaro umepitisha rasmi azimio la kuiomba Serikali kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kuwa jiji ifikapo mwaka 2015.
Azimio hilo limepitishwa katika kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC), chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa, Leonidas Gama ambaye amewataka watendaji wa ngazi mbalimbali kutekeleza vigezo vichache vilivyobaki ili kupandishwa hadhi hiyo
↧