Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha
tabia ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na
kudai wanaziendekeza wao wenyewe.
Akiongea na mwandishi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi
kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi
huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia
zinavyowasukuma.
↧