Siku chache baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii
wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji
tena mwanaume kwani anajikita zaidi katika kufanya kazi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Rose alisema katika maisha yake
ya uchumba alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya
mtoto hivyo anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.
↧