Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini
yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza
mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku
ambayo Rais huo atatua nchini.
↧