CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema watendaji waliohusika kusababisha mgogoro katika Kiwanda cha Chai Mponde, kilichopo Jimbo la Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, wanapaswa kuwajibishwa pamoja na kuachia ngazi.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mponde, Jimbo la Bumbuli, wilayani humo.
↧