Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea
meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza
ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana
wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu
ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
↧