Matumizi ya dawa za kienyeji kwa ajili ya kuongeza uchungu na kujifungua mapema, imeelezwa kuchangia zaidi vifo kwa wajawazito.
Mganga Mkuu wa Mkoa Kigoma, Dk Leonald Subi alisema hayo mjini Kigoma kwenye kikao cha wadau wa afya.
Kikao hicho kilihusisha kufanya tathmini na kuona hatua za kuchukua kukabiliana na vifo vya wajawazito na watoto wakati wa kujifungua mkoani humo.
↧