MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe amesema kiongozi yeyote ndani ya chama hicho ambaye ataruhusu
mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi bila kupingwa
atashughulikiwa.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua uchaguzi wa Baraza la
Vijana la Chadema (BAVICHA) uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City,
jijini Dar es Salaam.
↧