WATOTO watatu wa familia moja, wakazi wa Nyankumbu, Wilaya ya Geita, mkoani Geita, wamefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto uliowashwa kwa mafuta ya petroli na mtu asiyefahamika.
Dada mkubwa wa marehemu hao ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Sekondari Mwatulole na wazazi wao, walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo ambalo chanzo chake ni ugomvi
↧