Moto mkubwa umezuka kwenye jumba la Big Brother Africa Hotshots
katika studio za Sasani jijini Johannesburg, Afrika Kusini na hivyo
kuahirishwa kwa kuanza msimu mpya uliokuwa uzinduliwe Jumapili hii,
September 7.
Hakuna aliyeumia kutokana na moto huo uliotokea kwenye studio hizo
zilizopo Highlands North jijini Johannesburg jana Jumannne . Chanzo cha
moto huo bado hakijajulikana.
↧