JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ofisa Usalama wa Taifa feki ambaye amekuwa akijipatia fedha kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwahusisha na makosa yanayohatarisha usalama wa nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam; Kamishna Suleiman Kova, alimtaja ofisa huyo feki kuwa ni Saimoni Meena
↧