Hospitali ya Marie Stopes imemchagua Lady Jay Dee kuwa balozi wa
kampeni ya kuhamasisha uzazi wa mpango na kupinga mimba za utotoni
inayoitwa ‘Chagua Maisha’.
Akiongea na TBC, Lady Jay Dee amesema kuwa anaweza kufikisha ujumbe
kwa jamii kwa kuimba nyimbo ambazo zitasaidia kuwahamasisha wananchi
kuchagua jinsi ya kuishi kwa kutumia uzazi wa mpango.
↧