WAFANYABIASHARA wa maduka ya soko la Kariakoo wameanza mgomo kwa muda
usiojulikana kuanzia jana, sambamba na kuishinikiza Serikali kupunguza
kodi ya asilimia 18 wanayotozwa kupitia mashine za kielektroniki (EFDs).
Wamefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya TRA kutangaza
kufanya ukaguzi endelevu na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wale
watakaokaidi kutumia mashine hizo.
↧