Lady Jaydee ameamua kujibu habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku
la Risasi kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu
maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’.
Kwenye habari hiyo, Risasi wanadai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa
kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa
Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.
↧