Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha mwaka
mmoja jela Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Charles Ekelege na kumwamuru kurejesha Dola za Marekani 42,543
(Sh68,068,800).
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Augustina
Mmbando alimtia hatiani Ekelege baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na
mashahidi saba wa upande wa mashtaka, vielelezo
↧