Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imeanza mchakato wa kusikiliza
kesi dhidi ya Bunge la Katiba baada ya kupanga jopo la majaji wa
kuisikiliza.
Kesi hiyo namba 28 ya 2014, ilifunguliwa mahakamani hapo na mwandishi
wa habari, Saed Kubenea kupitia kwa Wakili Peter Kibatala, dhidi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi
ya mamlaka ya Bunge hilo.
↧