Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana
katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana
baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima
Mdee.
Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu,
Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda
ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo
↧