SAKATA la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutangaza nia ya kuwania urais,
limeibua mapya baada ya makatibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kudai
walipewa mafuta lita 60 na posho.
Wakizungumza jijini Mwanza jana kwa sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya makatibu hao walishangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, kudai kuwa hakukuwa na kikao hicho
cha siri.
↧