Wanajeshi 480 wa Nigeria wametorokea nchi
jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa
kundi la kiislamu la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali
Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa
silaha na sasa wamewekwa katika shule .
Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
↧