Maiti za watu 13 kati ya 16 waliokufa katika ajali ya mabasi yaliyogongana juzi mkoani Tabora, zimetambuliwa na ndugu zao.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 8 mchana katika kijiji cha Mlogolo wilaya ya Sikonge baada ya basi ya Am Coach na Sabena kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo na majeruhi 81.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alitaja waliokufa na
↧