Kituo maalum kilichotengwa kwa ajili ya kuwaangalia watu wenye dalili
za ugonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia kimeshambuliwa
na watu wasiojulikana waliopora vifaa.
Kwa mujibu wa BBC, tukio hilo lilifanyika usiku wa Jumamosi
iliyopita na watu takribani 30 walioliokuwa wamewekwa katika kituo hicho
kwa lengo la kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka.
↧