Vilio na simanzi jana vilitawala kwa wakazi wa maeneo ya
Sinai-Mabatini, baada ya vifo vya watu wanne wa familia mbili tofauti,
vilivyotokana na mvua iliyosababisha miamba mikubwa ya mawe kuporomoka
na kuponda nyumba zao usiku wa manane.
Tukio hilo la kusikitisha limeripotiwa kutokea saa nane usiku kuamkia jana, wakati mvua iliyoambatana na upepo wa wastani ilipokuwa ikiendelea
↧