Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuwawa kikatili
kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika katika eneo la
mkundi manispa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha
kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi
kufuatilia tukio hilo
↧