MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), amesema hatagombea ubunge kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwa kuwa amechoshwa na kauli za vitisho na kejeli dhidi yake, zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Amesema hayo jana kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wazee wa Mji wa Maswa na Malampaka wilayani humo, alipokuwa akijibu swali lao kuhusu
↧