Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia madai ya kutoka na msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na kudai kuwa wao ni washikaji tu ila ukaribu wao umesababisha mtifuano kati yake na mchumba wake, Siwema.
Akizungumza na mwandishi Nay alisema, watu wamekuwa wakieneza kuwa yeye na Wolper wanatoka kiasi cha kumkosesha amani Siwema na kufikia wakati f’lani wakatibuana.
↧