Kamishna Kova akiwa na RPC mpya wa Temeke, Kihenya Kihenya
*************
Jeshi la Polisi linamshikilia Inspekta wake, Celestine Makene
(40) kwa madai ya kumpiga hadi kumsababishia kifo mtoto wa kaka yake,
Alerd Makene (16).
Makene anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 24, mwaka
huu katika makazi ya polisi, Mtoni Kijichi, Dar es Salaam na
anashikiliwa katika Kituo cha Chang’ombe.
↧